ZILE TUZO MIYEYUSHO ZINAZOTANGAZWA NAMA MGAZETI NA VYOMBO VYAO VYA HABARI... ZINAENDESHWA HIVIIII... HEBU ONENI MFANO HAI...



 
Baada ya kutoka zangu kilingeni pale msasani club saa tatu(3) usiku nikainua simu ya mkononi kumpigia mmoja kati ya waendeshaji wa tamasha hilo:-
P The Mc: Haloo ndugu, naitwa P The Mc mmoja kati ya washiriki wa tuzo zenu.

JAMAA: Anhaa... eeeh....aanh sory kaka bado hatujamaliza kuhesabu kura zenu.

P The Mc: kikubwa sio kuhesabu kura, mimi nafikaje hapo na ni nani atakayenipokea nyie endeleeni na hesabu zenu.

JAMAA: sasa unajua tunahofia wote mkija hapa inaweza kuwa usumbufu ni bora tukishamjua mshindi tumpigie simu aje yeye tu peke yake.

P The Mc: Duuh! kwa hiyo mpaka nipige simu ndo mseme hivyo? nisingepiga ningejuaje? na huo mfumo mmeiga BET au GRAMMY? maana duniani sijajua kama kuna tuzo zinatolewa kwa mfumo huo

JAMAA: Usijali kaka we tuamini tu.

P The Mc: Hapana siwezi kuwaelewa hata kidogo, watu wametupigia kura kwa kulipia kila sms sh 250 kwa wote waliopiga kura ina maana haikupatikana hata pesa ya nauli ya kuwaalika wasanii wahusika?

JAMAA: (kimya...)

P The Mc: Mmetumia mfumo huo na kwenye category ya kina profesa j au ni category yetu tu?

JAMAA: (kimyaa..)

P The Mc: Nyinyi mliandaa hizo tuzo mkiwa na akili zetu au mlilewa kidogo?

JAMAA: Tafadhali usitukashifu kaka...

P The Mc: Siwakashifu bali nataka nijue

JAMAA: Tumeandaa tukiwa na akili timamu kaka

P The Mc: Sasa mbona mnaziendesha kama vichaa??

JAMAA: Kaka bado unatukashifu

P The Mc: (kwa hasira).. Sasa saa ngapi mtanipigia simu kuhusu hatima yake?

JAMAA: Saa tatu na nusu tu kaka.

Nikasubiria mpaka saa nne, kimya.

P The Mc: Haloo we jamaa...

JAMAA: Naam kaka

P the Mc: Vipi bado tu mnahesabu? au nyi wapuuzi mnataka kupindua matokeo

JAMAA: (kimya

P The Mc: Sasa mi naenda kulala mtanipigia simu kunipa matokeo..

SIMU HAIKUPIGWA MPAKA ASUBUHI HII...
shukrani sana kwa walionipigia kura,
May 26,2013 ahsanteni pia poleni kwa hatma mbovu ya jambo hili. Naheshimu sana mchango wenu kwenye sanaa yangu.

Maoni