KALA JEREMIAH AJIBU SHUTUMA BAADA YA KUDAIWA KUTOLIPA KURECORD DEAR GOD,

Mtayarishaji wa hit song ya Dear God, ngoma ya Kala Jeremiah na Producer Dee Classic akafunguka kuwa pamoja na ngoma hiyo ku hit na kumpa tuzo tatu Kala Jeremiah eti hajawahi kulipwa mtonyo kwa kutengeneza ngoma hiyo
Sasa Kala Jeremiah amejibu tuhuma hizi nzito dhidi yake na kusema Producer Dee Classic alikuwa mshkaji wake wa longy sana na walikuwa pamoja akiwa na beat zake akamwambia Kala achane mistari, kwahiyo haikua serious walifanya kama washkaji tu wanachana kwani Kala alikua na Dear God zamani sana na alifanya nae kama mshkaji na kusema kuwa hajapewa chochote atakua anakosea.

Maoni