SUGE KNIGHT APIGWA RISASI KATIKA PARTY PRE MTV VMA

Mkurugenzi wa zamani wa kampuni ya muziki ya Deathrow ya Marekani, Suge Knight anaripotiwa kufanyiwa upasuaji hospitali kufuatia kupigwa risasi katika sherehe isiyo rasmi ya tuzo za video bora za MTV.
Suge Knight inadaiwa alipigwa risasi kadhaa mapema siku ya Jumapili (Agosti 24), akiwa West Hollywood nightspot 1 Oak. Knight aliweza kuondoka huku akitembea mwenyewe katika sherehe hiyo iliyoandaliwa na Chris Brown, kabla ya polisi kumsaidia, kwa mujibu wa tovuti ya TMZ.

Maoni