Profesa Jay ametoa ushauri wake kwa wasanii wa Tanzania kutokubali kuwa chini ya mameneja ambao hawana taaluma hiyo.
Rapper huyo ambaye ameachia wimbo mpya ‘Tatu Chafu’, ameeleza kuwa meneja ni mtu ambaye anatakiwa kuwa mpiganaji anaemtafutia msanii njia za kutoka na kufanya shows nyingi kadiri iwezekanavyo na kwamba wasanii wengi wa Tanzania wamekuwa wakipenda vitu vya short-cut na ndio sababu wanafikia hatua ya kuangukia mikononi mwa watu wenye pesa wasio na taaluma ya umeneja.
Amesema hiyo ni sababu iliyomfanya yeye ashindwe kuwa na meneja na badala yake kuwa na washikaji ambao wanaweza kumsaidia kama marafiki badala ya kuwa na meneja ambaye anachofanya ni kulipia gharama za audio na video tu.
Maoni
Chapisha Maoni