Baadhi ya picha zikionesha wasanii wakiwa nyumbani kwa Afande Sele katika kumpa pole ya kuondokewa na aliyekuwa mkewe
Na hichi ndicho alichoandika Afande Sele "The King"
Napenda kuchukua fursa hii kipekee kuwashukuru kila mmoja wenu #marafiki #fans wote #ndugu #majirani #watanzania kwa umoja na mshikamano mliouonesha kwangu kipindi hiki kigumu sana kuwahi kutokea maishani mwangu kwa kuondokewa na mpendwa mke/mzazi mwenzangu. Sina maneno yanayoweza kuelezea kwa wepesi faraja, upendo na ushirikiano nilioupata kutoka kwenu, Nakushukuruni sana. ASANTENI.
Maoni
Chapisha Maoni