Rapa mkongwe wa bongo Profesa Jay wa mitulinga, kama unakumbuka vizuri tarehe 21 mwezi wa tano mwaka jana 2013 alikabidhiwa rasmi kadi ya uanachama wa chama siasa ch a Chadema na aliyemkabidhi Prof kadi hiyo ni mbunge ambaye pia ni msanii wa Hiphop Tanzania Joseph Mbilinyi/Sugu. baada ya pale hisia za watanzania zikasafiri mpaka mkoani Songea na kutoa jibu kwamba eti 2015 Profesa Jay anaenda kugombea ubunge katika moja kati ya majimbo ya mkoani humo, profesa jay nae akafunguka kuwa, yeye ameingia tu kwenye siasa kutaka tu kutumia sauti yake, kutumia kipaji chake na hali yake ya kujuana na watu kuweza kuwasaidia watu wengine kwa namna moja ama nyingine, hayupo kwa ajili ya kugombe sehemu yoyote.