Emmanuel Mbasha kujibu tuhuma dhidi yake za kumbaka shemeji yake

Emmanuel Mbasha, ambaye ni mume wa mwimbaji nguli wa nyimbo za Injili, Flora Mbasha amejitokeza hadharani na kusema kwamba atakwenda polisi mwenyewe kujibu tuhuma dhidi yake za kumbaka shemeji yake mwenye umri wa miaka 17
Faili la tuhuma dhidi ya
Mbasha lilifunguliwa Jumatatu iliyopita katika Kituo cha Polisi Tabata (Tabata Shule) wakati shemejiye huyo (jina tunalihifadhi), alipotaarifu kuwa Mbasha alimbaka mara tatu kwa siku mbili tofauti. Kesi hiyo ilipewa namba TBT/RB/3191/2014 na TBT/IR/1865/2014.

Maoni