Wamekubali promo kwenye show hata buku hawajalipwa(P The-mc Polymath)UKWELI ULIOFICHIKA



Wanadanganywa kwamba viduku ndo vinalipa/
Bado mazumbukuku na watupu kwenye vichwa/   
Ulimwengu uko huku unawaita/
Wamekubali promo kwenye show hata buku hawajalipwa/
Kuficha siri wanapiga picha na magari/
waonekane mziki ndo ushawalipa tayari/
gari za mapresenta, wanavishwa ufahari/
Wakati ukweli wamepigika hawana hali/
..........Ujanja kujituma bila noma/
Ukiwa mtumwa stori zitavuma kila kona/
Alosema wenzake wamebuma tumemwona/
Amepiga magoti kwa ustadhi juma na musoma/
Skia, enyi maboya hii ni habari kwenu/
Kwamba haiuzi bongo fleva, rap wala mayenu/
Mtavaa sana skin, kata sana mauno/
Mkishtuka mmefulia mnatuacha wabishi tumo/

Maoni