Hatuna haja ya kufichana tiba ni kuweka wazi,ukimwi ni upungufu wa kinga elimu kwa hiki kizazi,kuelimisha tukishindwa nani aokoe jahazi

Baada ya Juma kujua ni muathirika kulimuathiri kifkra siku moja akazidiwa akaona aiage familia,zikamjia hisia,akaamua kujisalia,akajiinamia huku Mungu akimlilia,kwa uchungu akamwambia,bado naipenda Dunia,akaanza kuomba-Nakushukuru kwa uhai,nitakufuru nikikudai,ingawa ninaumwa nina uhuru usiotozwa ushuru sishangai,kunidhuru haujawahi,umeninusuru tokea niko yai,uzima ni zaidi ya lulu dhambi zinaongezeka duniani hatujai,Mola mimi nateseka ukinilinda nitajidai,sikuchagua kupinda kuharibika hakufai,majaribu nimeyashinda shingo inakufa na tai,yote umeniwezesha ww ni muweza sikatai,ulimwengu unapendeza naomba uzima nifurahi,matumaini nitaendeleza niishi nitoe rai,sitorudia kucheza sitokunywa divai,akatia nia na imani, alikula si utani,matonge hayaishi kinywani,hana budi kuwa sawa,akawa anameza dawa,mwili ukarudi kibonge,siri juhudi asikonde,hakuitamani pombe,hata raia wachonge,asikonde asonge,uzani wa vidonge,mitihani ikampa donge,hakuna bingwa wa maradhi,hatuna haja ya kufichana tiba ni kuweka wazi,ukimwi ni upungufu wa kinga elimu kwa hiki kizazi,kuelimisha tukishindwa nani aokoe jahazi,wanaombukizwa sio wajinga waambieni watoto wazazi,muda wenu tumieni sio ukuda fundisheni haitoshi shuleni nyumbani wekeni jamvi,Juma bado anaishi afya njema sasa ni ustadhi,ametulia vyema anasa kwake haina hadhi,na huwa hasiti kuusema mkasa wake kwa baadhi.
Salu Tee

Maoni