MAONI NA USHAURI WA NASH MC ZUZU KWA MATAMASHA YA KILIMANJARO TOUR NA FIESTA

Miaka mingi sasa hakuna kitu kipya katika mfumo mzima wa show zenu hasa pale wasanii wanapokuja kutumbuiza,mashabiki hua tunajua tu kua msanii atapanda peke yake au siku hizi na wacheza show wake na ataimba kwa kufuatisha cd yake (PLAYBACK) kwa sehemu ndogo tu ya wimbo wake kisha baadae watacheza show na atashuka na kama ni wa kike atadili na suala la kukata viuno wanaume wamshangilie,kwa kweli mnawadumaza wasanii na suala la wao kwenda kimataifa silioni,angalieni utaratibu wa kuweka wasanii wachache na watakaokua na uwezo wa kupiga na Band au waambieni waache kuimba kwa kufuatisha cd zao (PLAYBACK) kwani inaonesha wazi hakuna ubunifu wala hamzingatii taratibu za muziki,msiangalie kutangaza biashara zenu au kuuza vinywaji vyenu pia muhusike ktk kuboresha na kuongeza ufanisi ktk kazi za sanaa,hasa muziki ambao mmejikita kutangazia kampuni zenu,kila napokaa kwenye tv nitazame wasanii wenzangu wanachofanya ktk show pengine ntajifunza kitu matokeo yake nazima na sipati chochote!
Haya ni maoni na ushauri wangu.

Maoni