Mwimbaji maarufu nchini Ghana Castro anaripotiwa kufa baada ya kujaribu kumuokoa msichana mmoja aliyeanguka ndani ya maji.

Polisi nchini Ghana wanatafuta mwili wa mwimbaji maarufu anayehofiwa kufa maji baada ya kupata ajali ndani ya maji. Msanii huyo, Castro wa miondoko ya Afrobeats anaripotiwa kufa baada ya kujaribu kumuokoa msichana mmoja aliyeanguka ndani ya maji karibu na hoteli moja iliyopo karibu na baharini. Chombo alichokuwa akiendesha (Jet ski) kimepatikana na polisi. Castro ambaye jina lake halisini ni Theophilus Tagoe alikuwa amerejea Ghana wiki iliyopita na alikuwa wakiburudika na nahodha wa Black Stars Asamoah Gyan, mabaye ni rafiki yake wa karibu.

Maoni