Diamond Ameeleza Utata Uliotokea Katika Tuzo Za Afrimma 2014 Tuzo hiyo Kupewa Mafikizolo.

Baada ya kutua katika uwanja wa ndege wa kimataifa wa wa Julius Nyerere, Dar es Salaam leo asubuhi, Diamond ameeleza utata uliotokea katika tuzo.
Amesema yeye alitajwa jukwaani kuwa mshindi wa tuzo mbili ya Msanii Bora wa kiume Afrika Mashariki na Wimbo Bora wa kushirikiana (My Number One Remix Feat. Davido), lakini baadae yalifanyika mabadiliko na tuzo hiyo kupewa Mafikizolo na wimbo wa Khona waliowashirikisha Uhuru.
Ameongeza kuwa hata Sheddy Clever pia alitajwa kuwa mshindi kama producer na kuoneshwa kabisa.

Maoni